• Moshi mkubwa ukifuka kutoka kwenye jengo la westgate mall Septemba, 23 ,2013.
  • Waokozi wa shirika la msalaba mwekundu wakikimbia nje ya ya jengo la Westgate Mall mjini Nairobi baada ya ufyatuaji wa risasi.
  • Vikosi vya usalama vya Kenya vikiwa nyuma ya ukuta nje ya jengo la Westgate Mall mjini Nairobi, Septembam, 23, 2013.
  • Watu wakichangia damu kwa watu waliojeruhiwa kwenye shambulizi katika jengo la westgate Mall.
  • Stephen , katikati, aliyempoteza baba yake katika shambulizi kwenye maduka ya westgate mall akifarijiwa na ndugu wakati akisubiri uchunguzi wa mwili wa baba yake. 
  • Raia waliokuwa wamejificha ndani wakati wa mashambulizi ya risasi walifanikiwa kutoka katika maduka ya westgate mall mjini Nairobi Septemba 21, 2013.
  • watu wakikimbia kutoka kwenye maduka ya kifahari ya WestGate Mall mjini Nairobi, Septemba, 21 2013.
  • Watu wakiwa wametoroka katika eneo la westgate mall mjini Nairobi, September 21, 2013.
  • Wanawake waliobeba watoto wakikimbia kutafuta usalama huku polisi wenye silaha wakiwasaka watu wenye silaha katika jengo la westgate Mall mjini  Nairobi, Septemba 21, 2013.
  • Mama na watoto wake wakiwa wamelala chini wakijifisha kuhofia watu wenye silaha katika jengo la maduka ya Westgate Mall mjini Nairobi Septemba, 21, 2013.

  Wanamgambo wa kiislamu wavamia maduka ya westgate Nairobi

  Published September 23, 2013

  Mwishoni mwa wiki wanamgambo wanaosadikiwa kuwa al- shabab walivamia maduka ya kifahari ya westgate mall mjini Nairobi. watu zaidi ya 60 wamekufa na wengine zaidi ya 175 wamejeruhiwa.