Multimedia

  • Watu wakikimbia kuokoa maisha yao baada ya milio ya risasi kulia Capitol Hill mjini Washington, D.C., Oct. 3, 2013.
  • Watu wakiwa wamelala chini kukwepa baada ya kusikia milio ya bunduki mjini Washington.
  • Polisi wakifuatilia hali hiyo Capitol Hill baada ya milio ya bunduki kuripotiwa karibu na mitaa ya 2nd Street NW na Constitution Avenue.
  • Polisi wa jengo la bunge wakiwa katika hali ya tahadhari Capitol Hill. (Diaa Bekheet/VOA)
  • Helikopta ya polisi ikiwa imembeba polisi aliyejeruhiwa inaondoka katika maeneo ya bunge Capitol Hill dakika chache baada ya risasi kulia. (Diaa Bekheet/VOA)
  • Watalii wakishangaa kufuatia tukio la upigaji risasi nje ya Capitol Hill. (Sandra Lemaire/VOA)
  • Bunge la Marekani lawekwa katika hali ya tahadhari baadaya risasi kulia karibu na majengo yake. (Diaa Bekheet/VOA)
  • Muonekano huu kutoka ofisi za jengo la Russell katika baraza la Seneti unaonyesha polisi wakikusanyika karibu na eneo la tukio. 
  • Wafanyakazi wa dharura karibu na maafisa polisi baada ya tukio hilo.
  • Polisi wa Capitol Hill na wafanyakazi wa huduma za afya wakimwondoa mtu aliyepigwa risasi katika machela.
  • Wafanyakazi wa dharura wakisaidia mtu aliyejeruhiwa.
  • Wafanyakazi wa uokozi wakiwa karibu na gari la polisi lililoharibika kufuatia ufyatuaji risasi karibu na Capitol Hill Washington.
  • Maafisa wa FBI wakifanya doria karibu na eneo ambapo milio ya risasi ilitokea.

  Milio ya Risasi yasikika nje ya Jengo la Bunge Marekani

  Published October 03, 2013

  Eneo la bunge la Marekani U.S. Capitol liliwekwa katika hali ya tahadhari Alhamisi mchana baada ya milio ya bunduki kuripotiwa nje ya jengo hilo, mtu mmoja inasemekana amejeruhiwa.