VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

21 Novemba 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Kibaki awaahidi wakenya katiba mpya

20/10/2009

Kenya's President Mwai Kibaki (undated photo)
Rais wa Kenya Mwai Kibaki.
Sherehe za mwaka huu za kuadhimisha mwaka wa 46 wa siku ya Kenyatta Day ziligubikwa na majonzi makubwa baada ya jengo la ghorofa tatu kuanguka ghafla katika mji wa Kiambuu katika viunga vya mji mkuu wa Nairobi, wakati wafanyakazi katika jengo hilo wakiendelea na ujenzi.
 
Licha ya maafa hayo mamia ya watu walifurika katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi katika sherehe za kuwakumbuka wapigania uhuru wa Kenya, pamoja na muasisi wa taifa hilo, marehemu Mzee Jomo Kenyatta.

Hotuba ya Rais Mwai Kibaki kwenye sherehe hizo iligusia zaidi suala nyeti la marekebisho ya katiba akasema kwamba juhudi zinafanywa na serikali ili kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana mwaka ujao.
 
Vile vile makamu wa Rais nchini humo bwana Kalonzo Musyoka aligusia suala hilo hilo la mageuzi ya katiba, akisema ana hakika katiba mpya itandikwa. Waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga hakuhudhuria sherehe kwa sababu yuko ziarani China.


Download Kibaki katiba
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Kibaki katiba
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya

  Mahojiano zaidi