VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

21 Novemba 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Burundi inawatia kizuzini mabalozi wake wawili

27/10/2009

Mabalaozi wawili wa Burundi, yule anaeiwakilisha nchi mjini Nairobi, Kenya, na yule wa Rome, Italy, walikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbiura walipowasili, kwa  tuhuma za wizi wa maelfu ya dola zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya ofisi za balozi hizo.

Serekali ya Burundi hapo mwanzoni iliwaita nyumbani mabalozi hao, lakini maafisa wa usalama waliwakamata walipowasili na kuwaweka kizuizini mara moja. Hatua hiyo imewakera watu wengi na wapinzani nchini kwa vile mabalozi hao walikua maafisa wa vyeo vya juu wa serekali na hawakupewa kinga za za kibalozi au haki ya kufikishwa mahakamani.

[insert caption here]
Pacrase Cimpaye
Pancrase Cimpaye msemaji wa chama cha Fredebu alizungumza na Sauti ya Amerika na kusema kuwa hatua iliyochukuliwa na serikali ina ushawishi wa kisiasa na wala haihusiana na suala la wizi wa fedha.

Anasema ikiwa ilihusiana na ulaji rushwa basi huko huko Bujumbura kuna watu wengi wanaopora mamilioni ya dola na kuachiwa huru ukilinganisha na fedha zinazodaiwa kuchukuliwa na mabalozi hao ambazo amesema ni kidogo mno.

Bw Chimpaye ameongeza kusema kuwa upinzani haungi mkono hatua hiyo kwa vile ni kinyume cha sheria na haikufuata taratibu za mahakama. Anasema huwenda inatokana na mvutano wa ndani wa chama ambapo wanachama wengi hawaridhiki na uwongoizi wa chama.


Download Brundi Mabalozi
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Brundi Mabalozi
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mapya

  Mahojiano zaidi