VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

22 Novemba 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
AU yajaribu kutanzua mzozo wa Madagascar

04/11/2009

Andry Rajoelina addresses supporters at a rally in Antananarivo on 02 Feb 2009
Andry Rajoelina rais wa Madagascar
Rais wa sasa wa Madagascar Andry Rajoelina, alikaa upande mmoja wa ukumbi mkubwa wa Umoja wa Afrika. Nae rais aliyemng’oa madarakani mapema mwaka huu, Mark Ravalomana, alikaa upande wa pili wa ukumbi huo.
Hawakupeana mikono, wala hawakutowa hata ishara ya kutambua kuwepo kwa mwengine kwenye mkutano huo.

Marais wengine wawili wa zamani Didier Ratsiraka na Albert Zafy, pia walikuwemo katika ukumbi huo, kadhalika mwenyekiti wa kamisheni ya AU Jean Ping, ambaye aliwakumbusha kwamba madhara ya kiuchumi na ya kisaikologia yanawaathiri raia wa Madagascar, kwa kuchelewesha kwao kutatuwa mzozo huo wa kisiasa.

Amesema “Ukweli kama unavyo ujuwa, huko Madagascar, unatambulishwa na machofu ambayo watu wa Madagascar wanahisi, watu ambao wanataraji mzozo utamalizika. Mzozo ambao watu wote wamesozwa. Na hali ya kiuchumi na kijamii nchini kwenu inazidi kudumaa kila siku. Watu wa Madagascar wanastahiki maisha bora ya baadaye, na hilo linawategemea nyinyi.”

Bw. Ping aliwaambia vyama hivyo vinne,kwamba watahukumiwa vikali iwapo watakosa kufikia maelewano juu ya kuundwa kwa serikali ya mpito, ambayo itapelekea kuandaa uchaguzi mpya mwakani.

Lakini matamshi walotoa  viongozi wanaohasimiana,kabla ya mkutano huo kuanza, yanaonesha majadiliano yanakabiliwa na changemoto kubwa.
Rais wa Madagascar aliyepinduliwa Marc Ravalomanana  18 May 2009
Rais wa Madagascar aliyepinduliwa Marc Ravalomanana 18 May 2009

Bw. Rajoelina alinukuliwa akisema kabla ya kuondoka Antananarivo,kwamba yeye hatotoa ridha zaidi ya alizotowa wakati wa mikutano ya awali yalofanyika huko Msumbiji.
 
Nae Bw. Ravolamana alisaema hapo mapema kwamba yeye hatokubali kushiriki kwenye majadiliano hadi pale  Rajoelina, ameondoka kwanza kutoka madarakani.


E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya

  Mahojiano zaidi