VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Somalia Yakanusha Kuingia tena Majeshi ya Ethiopia

21/05/2009

Islamic fighters take up positions as they fight pro-government fighters in Mogadishu, 10 May 2009
Wapiganaji wa Kiislam nchini Somalia
Ripoti kutoka Somalia zinasema wanajeshi wa Ethiopia wamerudi nchini humo kujaribu kurejesha hali ya usalama baada ya waasi wa nchi hiyo kuzidisha mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Lakini Waziri wa Habari wa Somalia Farhan Ali Mohamud anasema serekali imesikia ripoti hizo kutoka vyombo vya habari kuwa majeshi ya Ethopia yameingia lakini anasema hadhani ni ripoti sahihi.

Hatahivyo alisema  inaeleweka kwa Ethopia kupeleka wanajeshi wake kwenye mpaka  kujilinda kutokana na kuendelea kwa vita i upande wa pili wa mpaka ndani ya  Somalia. 

Majeshi ya Ethopia yaliondoka mwezi Januari mwaka huu baada ya makubaliano ya amani kufikiwa kati ya serekali na kundi la Rais Sharif Sheikh Ahmed katika upinzani, lakini Ethopia ilisema majeshi yatarudi ikiwa maslahi yake yako hatarini.

Ethopia ina kikosi kikubwa cha wanajeshi kwenye mpaka wake. Serekali ya Ethopia imekanusha kwamba wanajeshi wake wameingia nchini humo. Tangu May 8 wanaharakati kutoka makundi ya al-Shabab na Hizbul Islam, mungano wa wanamgambo wamekua wakipambana na majeshi ya serekali na wanamgambo wanaoiunga mkono serekali na majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.


Download Mapigano Somalia
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Mapigano Somalia
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Suala la Ardhi EAC Lafafanuliwa  Audio Clip Available

  Mahojiano zaidi
Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu
CUF yafurahishwa na hotuba ya Karume  Audio Clip Available
Israel na Misri zatoa mwito wa amani
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available