VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Waislamu Kenya walaani ugaidi

22/06/2009

Ciidamada Al-Shabaab
 Al-Shabaab
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kigaidi nchini Somalia na Kenya. Serikali ya Kenya imeanza kuchunguza madai kuwa vijana wanaanza kuandikishwa kujiunga na kundi la kigaidi la Somalia Al-Shabaab.

Lakini nchini Kenya, inaripotiwa mkenya kwa jina Saleh Ali Saleh Nabhan anaongoza kundi lake la kigaidi lenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al Qaida kwa jina Al-Muhajirun. Kundi lake hilo yaripotiwa lina wapiganaji waliopewa mafunzo nchini Afghanistan na Pakistan.

Akizungumza na sauti ya Amerika kutoka Mombasa, mwenyekiti wa baraza kuu la mashauri la waislam wa Kenya Sheikh Juma Ngao, alisema viongozi wa dini ya kiislam wanajiandaa kutoa hamasa kwa waislamu kote nchini humo kupitia misikiti na madrassa kuwaelezea vijana misingi na nguzo za dini ya kiislam ambayo inalaani vikali vitendo vyote vya kigaidi.

Aidha Sheikh Ngao alisema hivi karibuni baraza lake litaanda kukutana na familia ya Saleh Nabhan kusikiliza maoni yao na kutoa ushauri kwao kufutia tendo la kijana huyo kujihusisha na vitendo vya kigaidi. Nabhan anatuhumiwa kuhusika na jaribio la kutungua ndege ya Israel ikiwa katika anga ya Kenya na hoteli ya Paradise mjini Mombasa .

Na kuhusu ombi la Somalia kuzitaka nchi jirani za Kenya, Djibouti, Ethiopia na Yemen kupeleka majeshi yao kusaidia serikali dhaifu ya Somalia, Sheikh Ngao alisema haungi mkono ombi hilo. Alisema kupeleka majeshi hayo nchini Somalia ni kuhatarisha maisha yao bure na kwamba tatizo la kisiasa la Somalia linapaswa kutatuliwa na wasomalia wenyewe, kwani ni watu wa kabila moja, lugha moja na dini moja.


Download Viongozi wa kidini walani ugaidi
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Viongozi wa kidini walani ugaidi
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala zaidi
Somalia Yakanusha Kuingia tena Majeshi ya Ethiopia
 
  Makala mepya
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni

  Mahojiano zaidi
Jenerali Kazini wa Uganda auawa na mpenzi wake
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Maharamia wa Somalia washambulia Meli Bahari ya Mbali
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
MDC yatoa siku 30 za suluhisho Zimbabwe
Ocampo ataomba uchunguzi kuhusu ghasia Kenya
Warepublican na Wademocratic watofautiana juu ya ushindi Marekani  Audio Clip Available
Wakimbizi wa Congo warudi nyumbani
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available
Operesheni "rudi nyumbani" Kenya yaingia dosari  Audio Clip Available
AU yajaribu kutanzua mzozo wa Madagascar
Wauaji wa Albino wahukumiwa vifo  Audio Clip Available
Kabila atafuta suluhisho kwa Zimbabwe
Makundi ya kutetea haki Zimbabwe yasusia mkutano wa serekali.
Viongozi wa AU waizungumzia mzozo wa Darfur
Habari kuu Kenya na Marekani wiki hii  Audio Clip Available
Marekani yaiwekea Sudan vikwazo
Msumbiji wapiga kura kwa amani
Burundi inawatia kizuzini mabalozi wake wawili  Audio Clip Available
Rais Mugabe na Tsvangirai washindwa kuelewana
Marekani inamnyima afisa wa juu Kenya visa  Audio Clip Available
Kampeni za uchaguzi mkuu Msumbiji za pamba moto
Mkataba mpya wa waliopoteza makazi Afrika
Kiongozi wa Mungiki aachiwa huru  Audio Clip Available
Afrika kusaini makubaliano kuwalinda wakimbizi
Al-Shabab wajaribu kumshambulia rais wa Somalia  Audio Clip Available
Guinea kupelelezwa kwa kukiuka Haki za Binadamu
Wakfu wa Mandela Wakanusha Madai
Jumuia ya kimataifa haiwasaidi IDP's wa Somalia
Kibaki awaahidi wakenya katiba mpya  Audio Clip Available
Hakuna anayestahili tuzo la Mo Ibrahim 2009
MDC yaacha kujihusisha na serikali ya Umoja ya Zimbabwe
Ghana yachukua kombe la Dunia chini ya miaka 20
Afrika Mashariki yazidi kukumbwa na njaa  Audio Clip Available
Dunia yamkumbuka Mwalimu  Audio Clip Available
HRW yaishutumu DRC kutowajali raia wake
Obama apokea kwa mshangao na unyenyekevu tunzo ya amani  Audio Clip Available
Waathirika wa Mabomu 1998 Tanzania waandaa Kesi  Audio Clip Available