VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Wanawake wabakwa jela Goma

23/06/2009

Umoja wa Mataifa unaripoti kwamba zaidi ya wanawake ishirini walibakwa na wafungwa wanaume katika gereza kuu la mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Afisi ya Umoja wa Mataifa huko Congo MONUC, imeleza hakuna mfungwa aliyeweza kutoroka kutoka jela hiyo. Wanawake 20 walibakwa na kuteswa na wafungwa hao ambao ni wanajeshi waliokua wamekamatwa kwa utovu nidhamu. 

Hundreds of women demonstrate in central Brussels, Belgium, against women rape in the Democratic Republic of Congo, 26 Nov 2007
Mamia ya wanawake waandama Brussels dhidi ya ubakaji

 Akizungumza na sauti ya Amerika kutoka Goma, mtetezi wa haki za binadamu Bi Janine Bandu alisema alisikitika sana kuwaona wafungwa hao wa kike walivyoathirika. Alisema baada ya kubakwa na wafungwa wenzao, waliwekwa vyombo kwenye sehemu zao za uzazi na kupelekwa kwa matibabu katika hospitali za Goma.

Mtetezi huyo wa haki za binadamu anasema tatizo la ubakaji na manyanyaso dhdii ya wanawake limekuwa sugu, na kwamba mwanamke nchini Congo yumo katika hatari ya kubakwa wakati wowote ule. Bandu alikemea kitendo hicho kiovu na kuiomba serikali na wafadhili kutetea maslahi ya wanawake nchini humo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa afisa mmoja wa polisi aliuwawa pamoja na wafungwa watatu na walinzi wasiopungua tisa kuijeruhiwa baada ghasia hizo kuzuka katika gereza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi gereza hilo lilikuwa na wafungwa 837 ambapo 512 ni askari na wanajeshi wanaozuiliwa kutokana na makosa mbali mbali.

Umoja wa Mataifa umewataka wafungwa waliohusika na ghasia hizo na vitendo hivyo viovu waadhibiwe vikali na wakuu wa nchi wafanye mageuzi katika magereza yao pamoja na kuwatenga kabisa wafungwa wa kiume na wale wa kike.


Download Wanawake wabakwa Goma
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Wanawake wabakwa Goma
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Marekani na India kuimarisha ushirikiano wao

  Mahojiano zaidi
Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu
Suala la Ardhi EAC Lafafanuliwa  Audio Clip Available
CUF yafurahishwa na hotuba ya Karume  Audio Clip Available
Israel na Misri zatoa mwito wa amani
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available