VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Kenya yadaiwa kukiuka haki za binadamu


29/06/2009

The UN Special Rapporteur on extrajudicial executions, Philip Alston, address a press conference in Nairobi, 25 Feb 2009
Profesa Phillip Alston akiwasilisha ripoti yake
Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kuwa majeshi ya Kenya ikiwa ni pamoja na idara ya Polisi yalihusika na ukiukaji wa haki za binadamu katika maeneo mbali mbali ya jimbo la kaskazini mashariki hasa katika eneo la Mandera na kwenye maeneo ya mpaka wa Kenya,Somalia na Ethiopia. Watu walioathirika zaidi na ukatili huo wa jeshi la Polisi ni raia wa Kenya wenye asili ya Kisomali zaidi ya watu 1200 walijeruhiwa vibaya sana na mtu mmoja kuuwawa. Pia wanawake wasiopungua 12 walibakwa na maafisa wa jeshi la Polisi. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika hili la haki za binadamu ukatili ulifanywa na Polisi wakishirikiana na jeshi la nchi kavu walipokuwa katika heka heka za kuwasaka majambazi wenye silaha pamoja na wanamgambo wa kisomali wanaovuka mpaka na kuingia nchini Kenya. Hii si mara ya kwanza kwa mashirika ya haki za binadamu nchini humo kulaumu serikali ya nchi hiyo kwa kuhusika na ukatili na kukiuka haki za binadamu. Miezi kadhaa iliyopita mshauri wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Profesa Phillip Alston alitoa ripoti kali kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Kenya na akapendekeza kuondolewa madarakani kwa kamishna mkuu wa Polisi nchini Kenya Meja Jenerali Hussein Ali pamoja na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Bw. Amos Wacko.


Download Ukiukajihaki za Binadamu-Kenya
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Ukiukajihaki za Binadamu-Kenya
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Marekani na India kuimarisha ushirikiano wao

  Mahojiano zaidi
Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu
Suala la Ardhi EAC Lafafanuliwa  Audio Clip Available
CUF yafurahishwa na hotuba ya Karume  Audio Clip Available
Israel na Misri zatoa mwito wa amani
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available