VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Mkutano wa viongozi wa AU wafunguliwa

01/07/2009

Rais wa Sudan, Omar Hassan al Bashir atakuwepo katika mkutano huo akikaidi hati ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, waziri mkuu wa Italy, Silivo Berlusconni na rais wa Brazil Lula da Silava pia wapo kwenye orodha ya wageni. Lakini pengine habari kubwa ni kwamba rais wa Misri, Hosni Mubarak huenda naye akajitokeza.

Kiongozi huyo wa misri mwenye umri wa miaka 81 hajawahi kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika tangu kuepuka jaribio la kuuawa katika mkutano wa umoja wa nchi huru za afrika mwaka 1995 huko Addis Abeba.

Sauti ya amerika imeshindwa kupata visa ya kuhudhuria mkutano huo, lakini wanadiplomasia na waandishi wa habari  walisema mkutano huo unafanyika katika hali ya sherehe. 

Mkutano wa mwisho wa umoja huo uliofanyika Feburary ulihudhiriwa na viongozi 21 na kumuona Muammar Gadhafi akiapishwa. Kuna wasi wasi kuhusu idadi ya watakaojitokeza  huenda isiwe kubwa. Lakini bwana Gadhafi anazungumzia  kuwasilisha pendekezo lake la kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika, wengi ambao waliodhaniwa hawatafika pengine huenda wakahudhuria. 

African Union special envoy to Darfur Salim Ahmed Salim attends a meeting of Sudan's neighboring countries in the Red Sea resort of Sharm el-Sheikh 04 Dec 2007
Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu wa zamani wa OAU
Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu mkuu wa zamani wa OAU Bw Salim Ahmed Salim, alisema mbali na masuala ya kujitegemea upande wa kilimo na Afrika kuweza kujilisha wenyewe na masuala ya kiuchumi, anamini suala kuu litakua Darfur na migogoro mingine ikiwa ni Somalia, DRC, Madagascar na kadhalika.

 
Waandishi wa habari huko Sirte wanasema IGAD kundi linalojumisha nchi za Pembe na Mashariki Afrika zitauomba mkutano kubadili jeshi dhaifu la Umoja wa Afrika – AMISOM na kuwa jeshi lenye nguvu.

IGAD inajumuisha nchi sita za afrika Mashariki ambazo zinasemekana kuangalia  maamuzi ya awali ya kwazuia majirani wa Somalia kupeleka wanajeshi katika kikosi cha amisom. Ethiopia na kenya zinapakana na Somalia na zimekuwa zikiombwa kuwa na jukumu kubwa kwa jirani yao Somalia.


Download Salim Ahmed Salim
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Salim Ahmed Salim
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Marekani na India kuimarisha ushirikiano wao

  Mahojiano zaidi
Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu
Suala la Ardhi EAC Lafafanuliwa  Audio Clip Available
CUF yafurahishwa na hotuba ya Karume  Audio Clip Available
Israel na Misri zatoa mwito wa amani
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available