VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Dunia yamkumbuka Mwalimu

14/10/2009

Wakati Tanzania inadhimisha miaka kumi tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius 
Julius Nyerere
Baba wa Taifa wa Tanzania Julius Nyerere
Nyerere tarehe 14 Oktoba mwaka 1999, watanzania na ulimwengu mzima wanatoa maoni na hisia mbali mbali juu ya mchango wake na jinsi taifa lilivyo hii leo.

Wasomi na wanasiasa pamoja na wananchi wanamueleza Mwalimu kua alikua kiongozi aliyetetea maslahi ya taifa lake na wananchi wake, jambo ambalo halipatikani miongoni mwa viongozi wa leo.

Profesa Issa Shivji, mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salam, ameimabia Sauti ya Amerika kwamba cha ajabu ni kua mwaka huu kinyume na miaka ya nyuma, vyombo vya habari na wachambuzi wameanza kumzungumzia na kumjadili Mwalimu hasa katika sera zake za Azimio la Arusha.

"Kwa kweli kulikua na wakati ambapo watu walikua wanamzungumzia Mwalimu Nyerere bila ya kutaja Azimio la Arusha. Mimi ninaona hii ni muhimu sana na hii inaonesha kwa kiasi gani mfumo na sera zilizofuatwa baada ya yeye kun'gtuka, kwa kweli zimeonesha zimefilisika."

African Union special envoy to Darfur Salim Ahmed Salim attends a meeting of Sudan's neighboring countries in the Red Sea resort of Sharm el-Sheikh 04 Dec 2007
Salim Ahmed Salim
Salim Ahmed Salim, mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, anasema kwa ujumla mambo yale Mwalimu aliyapigania na kuyashikilia sana ni mambo yanaokumbukwa hasa na wananchi wa kawaida.

"Suala na unyonyaji wa mataifa makubwa kwa mataifa madogo linakumbukwa na wananchi wa kawaida wa Tanzania na linakumbukwa pia na wananchi wa Afrika. Ukweli ni kwambaj ambo hili limendelea na hasa katika dunia hii ya leo ya utandawazi, na matatizo yake na changamoto zake, watu wanakumbuka sana jinsi Mwalimu Nyerere alivyopigania haki za nchi changa kama Tanzania, kwa kuhakikisha kwamba angalau sisi tunapata haki katika jamii ya Kimataifa."


Download Nyerere Annivesary Shivji
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Nyerere Annivesary Shivji
Sikiliza (MP3)
Download Nyerere Annivesary Salim
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Nyerere Annivesary Salim
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available

  Mahojiano zaidi
Obama akamilisha ziara yake ya Asia
Marekani yazungumzia ugaidi Afrika
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Rais Obama awasili China kuimarisha uhusiano
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Habari kuu za wiki Tanzania na Rwanda
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Waliofariki na maporomoko Tanzania wazikwa  Audio Clip Available
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Ocampo ataomba uchunguzi kuhusu ghasia Kenya
Wakimbizi wa Congo warudi nyumbani
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available
Hakuna anayestahili tuzo la Mo Ibrahim 2009
Afrika Mashariki yazidi kukumbwa na njaa  Audio Clip Available