VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Marekani yaionya Zimbabwe kutokana na mivutano ya kisiasa

16/10/2009

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mashtaka ya ugaidi dhidi ya mbunge wa Zimbabwe Roy Bennet ni ukosefu mkubwa wa kisheria katika nchi hiyo ya Afrika.
 
Marekani pia inasema ni msaada wa kibinadamu pekee utakaotolewa kwa Zimbabwe, hadi serikali ya rais Mugabe itakapo kubali mabadiliko ya muafaka wa kushirikiana madaraka.

Utawala wa Obama unayashutumu mashtaka dhidi ya Roy Bennet kwa maneno makali, ukisema bayana kuwa hautoiga mfano wa Uingereza na kutowa msaada mpya kwa serikali ya muungano inayoongozwa na rais Mugabe.

Bennet ambaye ni mwanachama mwanzilishi na vilevile mweka hazina wa chama cha Movement for Democratic Change, katika serikali ya muungano alifungwa hiyo alhamis na kuamrishwa kufikishwa mahakamani kwa mashtaka ya awali ya kuwa na silaha za kigaidi kitisho kwa serikali ya Mugabe.

Chama cha MDC kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsangirai kinasisitiza kuwa Bw. Bennet hakutenda makosa kikisema kufungwa kwake ni tishio la kusudi la wafuasi wa chama cha Bw. Mugabe Zanu PF.

 


E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
CUF yafurahishwa na hotuba ya Karume  Audio Clip Available

  Mahojiano zaidi
Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu
Israel na Misri zatoa mwito wa amani
EAC yakubaliana juu ya soko la pamoja  Audio Clip Available
Hatari ya gesi katika Ziwa Kivu  Audio Clip Available
Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa  Audio Clip Available
Marais Obama na Hu wajadili uchumi kati ya Marekani na China
Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani  Audio Clip Available
Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar  Audio Clip Available
Mafuriko yaongezeka Tanzania  Audio Clip Available
Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika
Mapendekezo ya Katiba mpya Kenya kuchapishwa karibuni
WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya
Miaka 20 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin
Chanjo ya Malaria Yakaribia  Audio Clip Available