VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
Dunia yaungana kuisaida Haiti

15/01/2010

Interactive Forest

Waandishi wa habari wiki hii walizungumzia habari kuu, huku kipaumbele kikiwa ule mkasa wa tetemeko la ardhi lililotokea Haiti siku ya Jumanne.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Atlanta BMJ Mureithi alieleza kuwa vyombo vya Marekani vilitoa muda wake mwingi kuelezea janga hilo ambapo watu wanaokisiwa kuwa zaidi ya elfu 50 wamepoteza maisha yao. Mureithi alisema Rais wa Marekani Barack Obama aliongoza juhudi za jamii ya kimataifa kusaidia raia wa Haiti kwa hali na Mali.
 
Kutoka Kenya, mwandishi wa habari wa gazeti la Daily Nation Douglas Mutua, alielezea utata unaoendelea kumkumba waziri Mkuu bwana Raila Odinga anayeongoza juhudi za kupanda miche katika msitu wa Mau leo siku ya Ijumaa. Mutua alieleza kuwa Rais Mwai Kibaki alitazamiwa kushirikiana na bwana Odinga katika shughuli hiyo lakini ametoa sababu za kutokwenda kwenye msitu huo.

Baadhi ya wanasiasa wa mkoa wa Rift Valley wamehamaki kutokana na juhudi za bwana Odinga za kuhifadhi msitu huo baada ya wakazi haramu kutoka mkoa huo kufukuzwa kwenye msitu wa Mau.      
 


Download Habari Kenya na Haiti
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Habari Kenya na Haiti
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Kenya na Congo zatajwa katika ripoti ya haki za binadamu  Audio Clip Available

  Mahojiano zaidi
Ukarabati wa barabara ya Uganda na Rwanda waanza
Tahadhari yatolewa kuhusu uchaguzi Sudan
Afisa wa Marekani aomba msamaha kwa Libya
Bill Gates Ashuka Daraja katika Utajiri
Wakazi laki tano kuhamishwa Uganda
Baadhi ya maeneo Burundi yakumbwa na njaa  Audio Clip Available
Matukio ya Upigaji majumbani yaongezeka Kenya
Wakenya Wataka majina 20 ICC yafichuliwe  Audio Clip Available
Uganda yaongoza EA katika orodha ya FIFA
Sarkozy Akiri Makosa ya Ufaransa
Ratiba ya Kombe la Afrika 2012 Yapangwa
Wakili Marando:Babu Seya aweza kuokolewa tu na msamaha wa Rais  Audio Clip Available