VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

 
Habari katika Lugha 45
AU wamkatalia Ghadafi mwaka mwengine

01/02/2010

 Rais wa Libya Muammar Gadhafi amkubali kuondoka kama mwenyekiti wa Umoja wa mataifa 53 ya Afrika, lakini hakukubali kuondoka bila ya kutoa maneno makali dhidi ya umoja huo. Bw. Gadhafi aliwakemea viongozi wenzake kwa kukataa kuunga mkono mpango wake wa kuunda muungano wa mataifa ya Afrika.


Kwa juu juu mkutano ulipoanza ilionekana kana kwamba mambo yalikua mazuri. Viongozi wa mataifa ya Afrika waliingia kwenye ukumbi wa mkutano, na dakika 20 baadaye walitoka na kutangaza kwamba rais wa Malawi Bingu wa Mutarika atashika zamu kama mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika kwa mwaka huu. 
Rais wa Malawi Ck Bingu wa Mutharika.
Rais wa Malawi Ck Bingu wa Mutharika.

Lakini tangazo hilo lilificha ugomvi ulokuwepo ndani ya chumba cha mkutano, juu ya nani atachukuwa mamlaka ya umoja huo, uteshi ambao mashahidi wanasema ulikua nusra usababishe kutupiana ngumi miongoni mwa wajumbe usiku wa Jumamosi.

Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi alitazamia kuendelea kama mwenyekiti kwa awamu ya pili, ili kuona mpango wake wa muungano wa kisiasa na kiuchumi wa Afrika unatekelezwa. Lakini baada ya kumkabidhi kiongozi wa Malawi mamlaka ya mwenyekiti, bw Gadhafi katika hotuba yake ya kuaga, alitowa joto la roho, kwa kuwakashifu wenzake kwa ukosefu wa nia ya kisiasa.

“Si dhani tutaweza kuyabeba majukumu yanayotukabili. Si dhani kama tutaweza kukamilisha kitu muafaka katika siku zijazo kwa sababu nikizungumza kulingana na ujuzi wangu wa Umoja wa Afrika, viongozi wa bara hili wana upungufu wa uwelevu wa kisiasa na hivyo basi hawana nia ya dhati ya kisiasa.”

Bw. Gadhafi alijiita mwanajeshi wa Afrika, na kusema ataendelea na lengo lake la kuliunganisha bara hilo. Aliushambulia Umoja wa Afrika kwa kupoteza wakati kwa kutowa hotuba ndefu ndefu, maazimio, na matangazo, huku wakidharau dunia inayoendelea kubadilika.
Alisema kuna Umoja wa Ulaya ambao unabadilika na kua nchi moja na inafanyika kwa dhati.
Bw. Gadhafi alisema falau angelijuwa kuwa uwenyekiti wa AU una nguvu chache tu, basi angelikataa kuwa mwenyekiti wake.

Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika rais wa Malawi, Bingu Mutarika, alisema kuwa naye pia alikubaliana na baadhi ya malamiko ya bw Gadhafi.
“Njia mbele kwa mkutano mkuu wa AU, ni kutambua kwamba Afrika sio bara masikini, bali ni watu wake walio masikini. Hebu tuzingatie kwamba Ulaya na nchi nyingi za magahribi, ziliendelea mbele kwa kutumia mbao, nyama na samaki kutoka Afrika, lakini Ulaya na nchi za magharibi hazikuendelea kwa sababu ya maazimio na matangazo. Walichukuwa hatua. Hatua thabiti Kwa hiyo na wahimiza nanyi muchukuwe hatua, na hatua ziada na ziada.”


Kwenye kikao cha ufunguzi wa mkutano wa viongozi, katibu mkiuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon pia alitoa wito wa kushughulikiwa kwa haraka masuala muhimu ya bara hilo hasa changamoto za usalama huko Sudan na Somalia. Bw Ban alitoa wito pia kwa uungaji mkono mkubwa zaidi wa kimataifa kwa serekali ya mpito ya Somalia.


Download AU wamkatalia Ghadafi muda zaidi
Fungua  (MP3)
Listen to This Report AU wamkatalia Ghadafi muda zaidi
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya
Congress Marekani yapitisha mswaada wa afya

  Mahojiano zaidi
Obama ahimiza kupitisha mswada wa mageuzi ya afya.
Nigeria yakasirishwa na matamshi ya Gadhafi
Mahakama ya kimataifa yapinga rufaa ya Bikindi
Ghasia za kidini zaibuka tena Nigeria
AU ina wawekea vikwazo viongozi wa Madagascar
Jacob Zuma awasili Zimbabwe kutatua mzozo wa kisiasa
Wataalamu wa ukimwi eneo la IGAD wakutana Kenya  Audio Clip Available
Wabunge Kenya wamtaka Mudavadi ajiuzulu  Audio Clip Available
Wakimbizi wengi wa Sudan wamerudi nyumbani
Kenya na Congo zatajwa katika ripoti ya haki za binadamu  Audio Clip Available
Ukarabati wa barabara ya Uganda na Rwanda waanza
Tahadhari yatolewa kuhusu uchaguzi Sudan
Afisa wa Marekani aomba msamaha kwa Libya
Bill Gates Ashuka Daraja katika Utajiri
Wakazi laki tano kuhamishwa Uganda
Baadhi ya maeneo Burundi yakumbwa na njaa  Audio Clip Available
Matukio ya Upigaji majumbani yaongezeka Kenya
Wakenya Wataka majina 20 ICC yafichuliwe  Audio Clip Available
Uganda yaongoza EA katika orodha ya FIFA
Sarkozy Akiri Makosa ya Ufaransa