Abdushakur ni mtangazaji wa muda mrefu aliyejiunga na VOA 1992. Yeye ni mzaliwa wa Zanzibar lakini anatokea visiwani Comoro. Alihitimu uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Dakar, Senegal, na kupata mafunzo ya utangazaji wa Televisheni huko Ujerumani na Japan. Alifanyakazi na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, na baadae idhaa ya kiswahili na kingereza ya redio ya Uingereza BBC. Hivi sasa hutayarisha vipindi vya televisheni vya VOA pamoja na vipindi vya "Maswali na Majibu" na Muziki kutoka Afrika."