Majeshi ya Umoja wa Afrika yamepambana na wanamgambo  wa Somalia wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi wa  al-qaida  huko Mogadishu. Haikujulikana mara moja waliojeruhiwa  kwenye mashambulizi ya silaha nzito nzito  Jumanne alfajiri. Lakini maafisa wa kijeshi wanasema vikosi vya AU kutoka Burundi vikiungwa mkono na serikali ya mpito ya Somalia vilifanya mashambulizi kwenye ngome za al-shabab nje ya mji wa Mogadishu ili kudhibiti  mjihuo  wa Somalia. Walisema operesheni hiyo ilikuwa na mafanikio.