White house imesema imesikitishwa na kitendo cha Misri kuwazuia raia kadhaa wa Marekani kuondoka nchini humo.

Baadhi yao wameomba hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani huko Cairo wakati mvutano ukiongezeka kuhusu uchunguzi  wa serikali  kuhusu makundi ya demokrasia yanayopewa fedha  na nchi za nje.

Maafisa wa Marekani walisema jumatatu kuwa  Washington imezungumza suala hilo na maafisa wa kijeshi wa Misri na kuweka bayana  wasi wasi wao.

Msemaji wa White house Jay Carney amewaambia waandishi kuwa maafisa wanashughulikia kumaliza suala hilo haraka iwezekanavyo.