Mashahidi wanasema milipuko miwili imetokea katika mji wa kati wa Nigeria wa Kaduna Jumanne ikiwa mmoja karibu na kambi  ya jeshi.

Polisi walisema mlipuko mmoja ulitokea karibu na daraja na mwingine katika kambi  ya jeshi ya kitengo cha  ufundi nje kidogo ya Kaduna . Maafisa wanasema idadi ya waliojeruhiwa haijajulikana.

Polisi walikuwa wakichunguza ripoti kwamba mlipuko wa kwenye kambi ya jeshi ulisababishwa na mlipua mabomu wa kujitoa muhanga ambaye aliingiza gari mbele ya eneo la kuingilia.