VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

21 Novemba 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Operesheni "rudi nyumbani" Kenya yaingia dosari

03/11/2009

Jane (L) and Edward (R), Kenyan residents of the western Rift Valley district of Kiamba walk on through the burned out remains of a neighbors house. 19 Apr 2008
Watu waliopoteza makazi yao huko Rift Valley.
Hali ya wasiwasi imejitokeza katika eneo la Rift Valley nchini Kenya kufuatia uvamizi ambapo watu wawili waliuwawa huko Kuresoi siku moja tu kabla ya mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Luis Moreno Ocampo kuwasili nchini Kenya.

Watu hao wawili waliuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiojulikana lakini duru zinasema mauaji hayo yametokea baada ya vitisho dhidi ya wakimbizi kutolewa na kundi la watu wenye uhusiano wa karibu na baadhi ya washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi ambao wanakabiliwa na tishio la kupelekwa mbele ya mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC) huko nchini Uholanzi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Mwangi Geita anaripoti kuwa mamia ya watu ambao walikuwa wamerudi makwao kufuatia mpango wa serikali wa “operesheni rudi nyumbani” sasa wameanza kutoroka na kurejea kwenye makambi ya muda kufuatia tukio hilo, vitisho vya kuzuka kwa ghasia mpya na kuzorota kwa hali ya usalama kwa ujumla.


Download kenya idps
Fungua  (MP3)
Listen to This Report kenya idps
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mapya

  Mahojiano zaidi