• Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza na vyombo vya habari huko White House baada ya baraza la  Senet kupitisha muswaada wa kufungua tena baadhi ya shughuli za serikali  Oktoba 16, 2013.
  • Kiongozi wa walio wachache kwenye baraza la wawakilishi  Nancy Pelosi akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano wake na rais Barack Obama.
  • Rais Barack Obama akikutana na uongozi wa baraza la wawakilishi huko White House.
  • Spika wa bunge  John Boehner alipokutana na waandishi huko bungeni.
  • Seneta Charles Schumer mdemokrat kulia na kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la Seneti Harry Reid Mdemokrat Nevada walipozungumza na waandishi wa habari baada ya kupitishwa bajeti kwenye bunge la Marekani.
  • Watu wakiandamana dhidi ya kufungwa serikali nje ya jengo la serikali kuu huko  Los Angeles.
  • Spika wa bunge la Marekani   John Boehner akitokea kwenye mkutano na wawakilishi warepublikan huko bungeni, Oktoba 16, 2013.
  • Senata Ted Cruz Mrepublikan Texas akizungumza na waandishi wa habari huko bungeni Oktoba 16, 2013.
  • Mwakilishi  Devin Nunes  mrepublikan Carlifornia akizungumza na waandishi huko bungeni.
  • Kiongozi wa wachache Nancy Pelosi akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano wake na Rais  Barack Obama.

  Amerika yafungua shughuli za serikali 17 Oktoba 2013

  Published October 17, 2013

  Taswira mbali mbali Marekani ambapo ushindani kati ya warepublikan na White House juu ya bajeti ulisababisha kusimamishwa kazi kwa muda maelfu ya wafanyakazi wa serikali kuu tangu Oktoba mosi na wasi wasi kwamba siasa za mzozo ndio namna mpya ya kuongoza Washington.